Ticker

6/recent/ticker-posts

Kocha Yanga ahofia mziki wa Simba

KOCHA Kenny Mwaisabula amesema Dabi itakayopigwa Agosti 13, Yanga inatakiwa kukitazama kikosi cha Simba kwa jincho la tatu, kabla ya siku ya mechi.

Mwaisabula ambaye amewahi kuifundisha Yanga miaka ya nyuma, amesema ndani ya kikosi cha Simba kuna wachezaji wenye kasi, ambao wanaweza wakawa mwiba katika mchezo huo.

Amemtolea mfano Nelson Okwa, kwamba aliiona mikimbio yake Simba ilipocheza dhidi ya St.George iliyopigwa mabao 2-0 mechi ya kirafiki ya kimataifa katika tamasha lao.

 "Ni kweli Yanga ina kikosi kizuri sana na ina wachezaji wanaojua kumiliki mpira ambao kikawaida wanakuwa hawana kasi, hilo ndilo lililowagharimu dhidi ya Vipers ya Uganda," amesema na kuongeza;

"Ndani ya Simba ambacho hakijakaa sawa ni timu bado haijatengeneza kombinesheni, ila wana kikosi kizuri, natarajia utakuwa mchezo wenye ushindani mkali."

Post a Comment

0 Comments