Ticker

6/recent/ticker-posts

Nabi akiri Yanga Bado

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

"KOCHA Mkuu wa Yanga, Nesreddine Nabi, amesema anahitaji muda zaidi wa kutengeneza timu yake kwa kujenga muunganiko mzuri kati ya wachezaji wapya na wale waliobakia wa msimu uliopita baada ya kuona udhaifu wao kupitia mechi ya kirafiki dhidi ya Vipers ya Uganda." 

Hayo aliyazungumza juzi baada ya mchezo wa Yanga wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Vipers iliyoshinda mabao 2-0 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Wakati akihojiwa Nabi alisema mechi hiyo imekuwa kipimo kizuri kwa timu yake na amepata mwanga wa kuona baadhi ya vitu ambavyo anaenda kuvifanyia kazi.

Alisema ameona mapungufu ya kikosi chake, hivyo anahitaji kupata muda wa kutosha wa kutengeneza timu kwa wachezaji wapya na wazamani kupata nafasi ya kutengeneza muunganiko mzuri.

“Matokeo ya mechi yetu si mazuri, lakini kwangu nafurahi kuona nimepata kipimo tosha na vitu ambavyo natakiwa kufanyia kazi, wachezaji wapya na waliokuwapo msimu uliopita hawajapata muda wa kutosha wa kutengeneza muunganiko mzuri.

“Ninaamini hata mechi za mwanzoni hatutakuwa na ubora, kwa sababu nitatumia baadhi ya mechi za mwanzo wa ligi, muda huo utakuwa wa wachezaji wangu wote kuwa sawa, imara na kiufundi zaidi,” alisema Nabi.


Post a Comment

0 Comments