Ticker

6/recent/ticker-posts

Diogo Jota Aongeza Mkataba Liverpool Hadi Mwaka 2027

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Diogo Jota, 25, ametia saini mkataba mpya utakaomdumisha uwanjani Anfield hadi mwaka wa 2027.

Nyota huyo raia wa Ureno ameifungia Liverpool mabao 34 katika mechi 85 tangu ajiunge na Liverpool akitokea Wolves kwa €14M mnamo 2020.

Jota Amepachika wavuni mabao 21 msimu wa 2021-22 na kuiongoza Liverpool kunyanyua Kombe la FA na ubingwa wa Carabao Cup. Liverpool pia waliambulia nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA).

Hadi aliporefusha muda wa kuhudumu kwake Anfield, mkataba wa awali kati ya Jota na Liverpool ulikuwa utamatike mwaka 2025.

Mnamo Julai 2022, mshambuliaji mwingine wa Liverpool. Mohamed Salah, alisaini mkataba wa miaka mitatu  Anfield baada ya mshambuliaji Sadio Mane kuelekea Ujerumani kuvalia jezi za Bayern Munich.

Jota anatarajiwa kushirikiana pakubwa na Roberto Firmino, Mo Salah na sajili mpya Darwin Nunez katika safu ya mbele ya Liverpool baada ya Mane kuondoka.

Post a Comment

0 Comments