Ticker

6/recent/ticker-posts

Cristiano na Maguire wanaongoza orodha ya wachezaji wanao tukanwa zaidi mitandaoni

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Ronaldo na Harry Maguire ndio wachezaji wanaonyanyaswa zaidi kwenye Twitter kwa njia ya matusi, kulingana na utafiti mpya.

Utafiti huo ulifanywa na Ofcom na Taasisi ya Alan Turing ya nchini Uingereza, na iligundua kuwa Ronaldo, licha ya kuwa mfungaji bora wa Manchester United msimu uliopita akiwa na mabao 24, alipata dhuluma nyingi zaidi kwenye Twitter.

Angalau posti 60,000 za matusi zilipatikana zikielekezwa kwa wachezaji wa Ligi Kuu, na zote zilisambazwa katika msimu wa 2021/22.

Ronaldo alitumiwa ujumbe mwingi zaidi wa matusi kuanzia Agosti 13 na Januari 24, huku ujumbe mwingi 12,520 ukiwa na lengo la kumkashifu mshindi huyo mara tano wa Ballon d’or.

Nahodha wa United Harry Maguire alishika nafasi ya pili kwenye orodha hiyo, akiwa na angalau jumbe 8,954 za matusi zilizoelekezwa kwake katika kipindi hicho.

Twiti za matusi pia zilipatikana kuwaathiri wachezaji saba kati ya 10 wa ngazi za juu.

Wachezaji wengine waliokuwa kwenye 10 bora ya waliodhulumiwa zaidi mtandaoni ni pamoja na Marcus Rashford (2,557), Bruno Fernandes (2,464), Fred (1,924), Jesse Lingard (1,605), Paul Pogba (1,446) na David De Gea (1,394), wote kutoka Manchester United.

Harry Kane (2,127) na Jack Grealish (1,538) pia wameingia kwenye orodha hiyo.

Hivi karibuni, Cristiano Ronaldo amekuwa na ushirikiano mbaya na mashabiki wa Manchester United baada ya kueleza nia yake ya kutaka kuihama klabu hiyo.

Hata hivyo, baada ya kushindwa kupata klabu inayofaa kwenye Ligi ya Mabingwa, Ronaldo alirejea katika klabu hiyo na kushiriki mechi ya kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano Jumapili, Julai 31.

Post a Comment

0 Comments