Ticker

6/recent/ticker-posts

Christian Pulisic: Winga wa Chelsea Kujiunga na Man United Msimu Huu

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  • Christian Pulisic alikuwa amehusishwa pakubwa na tetesi za kuhama Stamford Bridge msimu huu akitafuta nafasi katika timu ya kwanza 

  • Raia huyo wa Marekani amekuwa akikumbana na hatima finyu chini ya ukufunzi wa Thomas Tuchel huku kocha huyo Mjerumani akiwapendelea Mason Mount na Raheem Sterling

  • Newcastle, Atletico Madrid, na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vikuu ambavyo vinamezea mate huduma za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.


Winga wa Chelsea, Christian Pulisic anaripotiwa kuwa kwenye mpango wa kuhamia klabu ya Manchester United msimu huu wa joto. 

Pulisic amekuwa akikumbana na wakati mgumu kuingia kwenye timu ya kwanza ya Blues chini ya ukufunzi wa Thomas Tuchel, na hivyo kumwacha bila budi ila kufanya uamuzi wa kuondoka.

Kwa mujibu wa ripoti ya Metro UK, mzawa huyo wa Marekani amekuwa akitafuta nafasi ya kufanya mazungumzo na Tuchel kumueleza wazi iwapo anahitaji huduma zake.

Inaaminika kuwa kuwasili kwa Raheem Sterling kumeathiri sana nafasi yake kwenye klabu ya Chelsea na hivyo ikihofiwa kwamba huenda atakosa kuchezeshwa na kutupwa mkekani. 

Ripoti zinadai kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amekuwa akiwazia hatima yake ugani Stamford Bridge huku akiviziwa na vilabu kama vile Newcastle United na Atletico Madrid.

Kocha wa Man United, Erik ten Hag pia anasemekana kuwa tayari kumuokoa kutoka kwa masaibu yake kwa kumpa suluhu ya muda ya kutua Old Trafford kwa mkopo. Hata hivyo, ripoti mpya zinadai kuwa haijulikana iwapo Pulisic atakamilisha uhamisho wake wa Old Trafford kama ilivyodaiwa awali. 

Daily Mail inaripoti kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, anatazamiwa kupiga abautani na kuamua kuchezea Chelsea akipigania nafasi katika kikosi cha kwanza. 

Pulisic pia anafahamika kuwa hataki kusubiri United, ambao wameweka kipaumbele kwa wachezaji wengine akiwemo Antony wa Ajax. 

Habari za hivi punde ni kuwa mustakabali wa Pulisic na Chelsea yanakuja siku chache baada ya kubainika kuwa Blues hawataki kumruhusu kujiunga na mpinzani wake wa karibu. 

Post a Comment

0 Comments