Hatimaye msimu mpya wa Ligi Kuu Uingereza (EPL) unatazamiwa kung'oa nanga wikendi hii baada ya mapumziko ya takriban miezi miwili.
Msimu wa EPL 2022/22 utaanza rasmi Ijumaa Agosti 5, 2022 na kuendelea kwa miezi kumi hadi Mei 28, 2023.
Mechi kati ya Crystal Palacena Arsenal ambayo itachezwa Ijumaa mwendo wa saa nne usiku ugani Selhurst Park ndiyo itakayofungua kalenda ya EPL 2022/23. Hiyo itakuwa mechi pekee ya EPL kuchezwa Ijumaa.
Jumla ya mechi sita za EPL zitachezwa siku ya Jumamosi katika viwanja mbalimbali nchini Uingereza.
Fulham ambao walipandishwa ngazi mapema mwaka huu watawaalika Liverpool ugani Craven Cottage mwendo wa saa nane unusu.
Mechi zingine nne zitachezwa Jumamosi mwendo wa saa kumi na moja zikiwemo Bournemouth vs Aston Villa, Leeds vs Wolves, Tottenham vs Southampton na Newcastle vs Nottingham Forest.
Everton na Chelsea zitafunga siku ya pili ya mechi za EPL katika mchuano ambao utachezwa saa moja unusu ugani Goodison Park.
Mechi tatu zitachezwa Jumapili kuanzia saa kumi alasiri.
Manchester United watakaribisha Brighton ugani Old Trafford huku wakati huo huo Leicester wakiwaalika wageni wao Brentford nyumbani King Power stadium.
Mechi ya mwisho kati ya West Ham na Manchester City itachezwa Jumapili mwendo wa saa kumi na mbili jioni katika uwanja wa Etihad Stadium.
0 Comments