Ticker

6/recent/ticker-posts

Utabiri wa Rio Ferdinand sita bora Ligi kuu Uingereza msimu huu


Gwiji wa  zamani wa Manchester United na mchambuzi wa BT Sport Rio Ferdinand atoa utabiri wake kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu ya Uingereza.

Rio Ferdinand anaamini Manchester City itatetea taji lao la Ligi Kuu msimu huu kutokana na "uzoefu wao wa kushinda".

Kikosi cha Pep Guardiola kilitwaa taji la msimu uliopita kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Aston Villa siku ya mwisho, na kufunga mabao matatu katika dakika 15 za mwisho Etihad na kumaliza pointi moja mbele ya wapinzani wao Liverpool.

Taji hilo lilikuwa lao la nne chini ya Mhispania huyo katika kipindi cha miaka mitano.

Klabu ya City sasa inadaiwa kuwa katika nafasi bora ya kushinda mataji mengi msimu huu baada ya kusajili Erling Haaland kutoka Borussia Dortmund na Kalvin Phillips kutoka Leeds.

"Nadhani City itakuwa timu ya kushinda tena," Ferdinand aliambia Mirror Football, kwa hisani ya BT Sport. "Wameimarika tena, wana Haaland na Kalvin Phillips. Wamempoteza Raheem Sterling, ndio, lakini wana kikosi kizuri bado na wachezaji ambao wanaweza kucheza nafasi nyingi. Na wanayo uzoefu wa kushinda. Liverpool  inafaa kujikaza sana uendapo wanataka kushindana nao.''

Kwa upande wa soka ya Ligi ya Mabingwa, Ferdinand alionekana kuiunga mkono  klabu ya United kuingia katika nafasi ya nne bora.

Mashetani Wekundu walimaliza katika nafasi ya sita kwenye Ligi ya Uingereza msimu uliopita  wakiandikisha pointi zao za chini zaidi (58) kwa miaka 32, na hawajashinda kombe lolote tangu Mei 2017.

Ferdinand pia anaamini kuwa klabu ya Tottenham itamaliza nafasi ya tatu, na kuziacha Chelsea na Arsenal nje ya nne bora.

Klabu ya Tottenham imetumia pesa nyingi msimu huu , kuwaleta Yves Bissouma, Ivan Perisic, Fraser Forster, Richarlison, Djed Spence na Clement Lenglet.

Klabu ya Arsenal pia imetumia pesa nyingi kuwasajili Oleksandr Zinchenko, Gabriel Jesus, Matt Turner, Marquinhos na Fabio Vieira.

Huku Chelsea ya Thomas Tuchel ikiwekeza pauni milioni 80 kuwanunua Raheem Sterling na Kalidou Koulibaly.

" Kwa sasa timu ambazo zina uwezo mdogo wa  kushinda ligi ni kati ya Chelsea, Manchester United na Spurs - na pengine Arsenal - kwa nafasi hizo za tatu na nne," anadai Ferdinand. "Nadhani hiyo itakuwa kinyanganyiro nzuri.''

Post a Comment

0 Comments