Ticker

6/recent/ticker-posts

Paula Kajala afunguka uhusiano wake na babake mzazi P-Funk Majani

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Mwanamitindo Paula Kajala ameweka wazi kuwa kuna uhusiano mzuri kati yake na baba yake mzazi P-Funk Majani.

Binti huyo wa muigizaji Kajala Masanja amefichua kwamba huwa anawasiliana na mtayarishaji huyo wa muziki na hata kuonana naye mara kwa mara.

"Tuko sawa. Kila siku tuko sawa. Tunaongea. Hata nilikuwa napanga kuenda kwake wiki iliyopita. Anakaa Arusha sasa hivi," Paula alisema Jumatano katika mahojiano na Wasafi Media.

Mwanamitindo huyo alidokeza kuwa mzazi huyo wake atahudhuria hafla ya 'Pink Friday Celebration'  ambayo ameandaa kufanyika Ijumaa.

Pia alifichua kuwa ataitembelea familia ya Bw Majani hivi karibuni na kubainisha kuwa kuna uhusiano mzuri kati yake na wadogo zake kutoka upande huo.

"Huwa tunaongea. Tunafanya video call. Tunazungumza. Huwa tunakutana mara nyingi. Hata nilikuwa naishi nao," Alisema.

Mwezi uliopita Bw Majani pia alifunguka kuhusu uhusiano wake na bintiye huyo wa miaka 20 na kuweka wazi kwamba huwa wanajuliana hali mara kwa mara na hata kukutana kwa wakati mwingine.

Mtayarishaji huyo akizungumza na waandishi wa habari mnamo siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Paula alimtakia binti huyo wa kheri na kumtaka afuate moyo wake katika shughuli zote za maisha.

"Nipo kwa ajili yake siku zote. Siku hizi tunaongea vizuri sana. Tunaenda vizuri na amekua. Ameanza kuwa mzima," Alisema Majani.

Mzazi huyo mwenza wa Kajala Masanja hata hivyo alifichua kuwa hakuna uhusiano mzuri kati yake na muigizaji huyo.

Majani alidai kuwa mchumba huyo wa sasa wa Harmonize amekuwa akipuuzilia ushauri  wake hasa kuhusu malezi ya binti yao.

"Paula bado mdogo, ana nafasi ya kubadilisha tabia. Mama yake yule hapana. Kwa kweli sisi hatuongei. Sihitaji kuongea naye tena!," Alisema.

Pia aliweka wazi kuwa kwa muda mrefu hakujakuwa na hali ya kuelewana kati yake na Kajala.na kufichua kuwa kwa sasa hata hazungumzi naye.

"Mama (Kajala) ni sumu. Lazima izingatiwe niko kwenye ndoa miaka nane na mtu ambaye nimekuwa naye miaka 12, kanizalia watoto watatu. Sasa kama mtu yuko na drama unamuepuka kidogo," P-Funk alisema.

Kwa sasa Majani yupo kwenye ndoa nyingine huku Kajala akipanga kufunga pingu za maisha na Harmonize hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments