Ticker

6/recent/ticker-posts

Man-City Wapewa Chelsea, Arsenal kukutana Na Brighton Katika Raundi Ya Tatu Ya Carabao Cup

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Manchester City, watavaana na Chelsea katika raundi ya tatu ya Carabao Cup msimu huu katika uwanja wa Etihad.

Chini ya kocha Thomas Tuchel, Chelsea walikamilisha kampeni za kipute hicho mnamo 2021-22 katika nafasi ya pili.

Pambano kati ya Man-City na Chelsea litakuwa moja kati ya saba yatakayokutanisha vikosi vya EPL katika raundi ya tatu ya Carabao Cup muhula huu. Limbukeni wa EPL, Nottingham Forest watamenyana na Tottenham Hotspur huku Manchester United wakimenyana na Aston Villa.

Washikilizi wa taji la Carabao Cup, Liverpool, watamenyana na Derby County inayoshiriki League One huku klabu za Newport County na Gillingham zinazonogesha League Two zikimenyana na Leicester City na Brentford.

Vinara wa EPL, Arsenal watakwaruzana na Brighton, Wolves watawaalika Leeds United, Newcastle United waonane na Crystal Palace nao Bournemouth wapimane ubabe na Everton.

Mechi za raundi ya tatu kwenye Carabao Cup msimu huu zitasakatwa kati ya Novemba 8-10, 2022.


DROO YA RAUNDI YA TATU YA CARABAO CUP 2022-23:

Leicester vs Newport County

West Ham vs Blackburn

Wolves vs Leeds United

Nottingham Forest vs Tottenham

Manchester United vs Aston Villa

Bournemouth vs Everton

Liverpool vs Derby

Burnley vs Crawley

Bristol City vs Lincoln

Manchester City vs Chelsea

Stevenage vs Charlton

MK Dons vs Morecambe

Newcastle vs Crystal Palace

Southampton vs Sheffield Wednesday

Arsenal vs Brighton

Brentford vs Gillingham

Post a Comment

0 Comments