Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga yaachana na Balama Mapinduzi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 𝗔𝗦𝗔𝗡𝗧𝗘 𝗕𝗔𝗟𝗔𝗠𝗔 𝗠𝗔𝗣𝗜𝗡𝗗𝗨𝗭𝗜

Tunashukuru kwa Mchango wako wenye mafanikio kwa Young Africans SC. Tunakutakia kila la kheri na mafanikio uendako.

𝗢𝗻𝗰𝗲 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝗻𝗰𝗵𝗶, 𝗔𝗹𝘄𝗮𝘆𝘀 𝗠𝘄𝗮𝗻𝗮𝗻𝗰𝗵𝗶


KLABU ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na kiungo mshambuliaji, Balama Mapinduzi 'Kipenseli' baada ya kandarasi yake kumalizika.

Balama alijiunga na Yanga Juni 22,  2019 akitokea Alliance ya Mwanza na kuonyesha kiwango kizuri ingawa majeraha ya mara kwa mara yalimfanya kushindwa kuwika hali iliyopelekea mabosi wa timu hiyo kuachana naye baada ya kudumu kwa miaka mitatu.

Licha ya majeraha yake ila ujio wa nyota wengine wapya kwenye kikosi hicho wakiwemo, Bernard Morrison, Gael Bigirimana na Aziz KI ungezidi kutishia nafasi yake ya kucheza.

Nyota huyo anakuwa wa pili kuachwa na Yanga msimu huu baada ya hapo awali kutangaza kuachana na Deus Kaseke ambao wote mikataba yao imeisha.


Post a Comment

0 Comments