Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga: Hakuna Wa Kumzia Fiston Kalala Mayele Msimu Ujao

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Yanga: Hakuna Wa Kumzia Fiston Kalala Mayele Msimu UjaoTimu ya Yanga imeibuka na ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Transit Camp katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jana Ijumaa, Julai 29, 2022.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa Yanga katika maandalizi ya kuuanza msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC inayotarajiwa kuanza kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba mnamo Agosti 13, 2022.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Fiston Kalala Mayele ambaye amepiga hat-tirick (mabao matatu), Stephane Aziz KI amefunga bao moja na Heritier Ebenezer Makambo ambaye pia amefunga bao moja.

Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2021/22 wameweka kambi yao katika maskani yako yaliyopo Avic Town Kigamboni Dar, huku mahasimu wao Simba wakijichimbia katika mji wa Ismailia nchini Misri.

Post a Comment

0 Comments