Ticker

6/recent/ticker-posts

YANGA: Nasreddine Nabi Ampongeza Gael Bigirimana Asema ni Zaidi ya Kiungo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


KOCHA Mkuu wa YANGA Nasreddine Nabi baada ya kawaangalia mastaa wapya waliosajiliwa msimu huu wakati timu hiyo ikiendelea kujifua kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi huku ikifuata ratiba ya mazoezi mara mbili kwa siku kocha Nabi amemwangalia kiungo mpya Bigirimana na kusema ‘Huyu Gael Bigirimana kuja Yanga ni zaidi ya bonasi.’

Kocha Nabi alisema ameamuangalia Bigirimana kwa umakini na kutambua kwamba jamaa ni kiungo aliyekamilika anayejua kufanya kazi yake vyema eneo la kiungo.

Nabi aliongeza kwamba pasi za Mrundi huyo pamoja na akili yake ya kukaba kisasa vitaiongezea Yanga kasi kubwa eneo la kiungo msimu ujao.

“Ni mtu aliyekamilika sana, nafikiri uamuzi wake wa kuja Yanga ni kama tumepata dhahabu kubwa ambayo itatupa mabadiliko makubwa katika kikosi chetu,” alisema Nabi.

“Nafikiri sio tu mashabiki wataburudika na ubora wake lakini pia hata wachezaji ambao watamuangalia kuna vitu watajifunza, anavyocheza ndivyo kiungo wa kisasa anatakiwa kucheza, ukiona jinsi anavyokaba na kupiga pasi nafsi yako inatulia.”

Aidha, Nabi amesisitiza kwamba hakuna staa kwenye kikosi chake na kwamba kwasasa wanakwenda kutengeneza timu mpya.

Kocha huyo aliyechukua tuzo ya kocha bora pamoja na kuiwezesha Yanga kuchukua mataji matatu msimu uliopita, alisema kitu kikubwa kitakachompa nafasi mchezaji ni uwajibikaji wake mazoezini na sio jina lake.

Nabi alimaliza kwa kusema “Nafurahi kuona wachezaji wanapambana sana.”

Post a Comment

0 Comments