Ticker

6/recent/ticker-posts

VIDEO: STEPHANE AZIZ KI ATUA YANGA

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

AFISA Habari wa Klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa mchezaji Stephen Aziz Ki tayari ameshatua nchini Tanzania kama mchezaji mpya wa klabu hiyo.

Bumbuli: Aziz Ki alikwisha malizana na Yanga tangu muda mrefu kilichokuwa kinasubiriwa ni yeye kumalizia msimu akiwa na klabu yake aliyokuwa akiichezea msimu uliopita ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.

“Aziz Ki ni mwananchi kwa asilimia 100 nduguyangu wana Yanga wasiwe na wasiwasi, sema watu wanasahau haraka sana na sijui kwanini wanasahau au sijui waandishi mnawasahaulisha! Tulishatoa taarifa mapema mara baada ya Rais Injini Hersi kwenda kumalizana naye kule tulithibitisha kuwa ni mwananchi na ameshasaini kandarasi ya kuitumikia Yanga.” Amesema Bumbuli

Klabu ya Yanga hadi sasa imekwisha kamilisha dili za usajili wa wachezaji watano wa kigeni akiwemo Lazarous Kambole, Bernard Morrison, Gael Bigirimana pamoja na Joyce Lomalisa Mutambala na Aziz Ki.Post a Comment

0 Comments