Ticker

6/recent/ticker-posts

Arsenal Yashauriwa Kuwinda Saini Ya Youri Tielemans

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Arsenal Yashauriwa Kumsajili Youri Tielemans wa Leister city

Arsenal itawafurahisha mashabiki wao ikiwa watamleta Youri Tielemans.

Hayo ni maoni ya Noel Whelan ambaye anadai kiungo huyo wa Leicester angeingia kwenye kikosi cha Arsenal ili kukiimarisha zaidi.

Aliiambia Football Insider: "Pauni milioni 30 kwa mchezaji kama Tielemans, wakati unajua anaweza kufanya hivyo kwenye Ligi ya Premia - sio kitu.

"Nadhani angefaa moja kwa moja kwenye mtindo wa uchezaji wa Arsenal, na mashabiki wangefurahi sana kama wangempata.

"Ni mchezaji wa kiungo mwenye kipaji kikubwa, na kama unaweza kumpata kwa bei ya aina hiyo basi bado watakuwa na bajeti ya kutoka na kupata winga pia.

“Naamini angekuwa mmoja wa viungo bora ambao wamekuwa nao kwa muda mrefu. Ningependa kumuona klabuni, kwa hakika."

Post a Comment

0 Comments