Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za usajili: Martial kusalia Man Utd; Barcelona wamtolea macho Laporte

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag amekataa kumuuza Anthony Martial msimu huu wa majira ya joto. Mfaransa huyo amefunga mabao matatu katika mechi tatu za kujiandaa na msimu mpya.


Donny van de Beek ni mchezaji mwingine ambaye hataruhusiwa kuondoka United baada ya kurejea akitokea Everton kwa mkopo.

Barcelona wanawania kuinasa saini ya beki wa kati wa Manchester City, Aymeric Laporte iwapo watashindwa kumnasa Jules Kounde wa Sevilla.

Chelsea wamefikia makubaliano na Sevilla ya kumsajili beki Kounde baada ya chelsea kutoa dau nono la usajili na tayari wamekubaliana maslahi binafsi na atasaini mkataba wa miaka mitano.

Liverpool wameingia tena sokoni kusaka saini ya kiungo wa Sporting CP Matheus Nunes wapo tayari kutuma ofa ya pauni milioni 43 kabla ya kumalizika kwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Real Madrid wamekanusha taarifa za kutaka kumsajili mshambuliaji mkongwe Edin Dzeko kutoka Inter. Pia hawana mpango tena na Cristiano Ronaldo, ambaye yuko tayari kupunguziwa mshahara ili aondoke Manchester United.

Ofa ya Manchester City ya pauni milioni £30m ili kumnunua beki wa pembeni wa Brighton & Hove Albion Marc Cucurella Imekataliwa. The Seagulls wapo tayari kumwachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa pauni milioni £50m.

Arsenal na Everton zote zimekataa nafasi ya kumsajili winga wa Atletico Madrid Thomas Lemar kwa mkataba wa kudumu.

Ofa ya Tottenham ya pauni milioni £25m pamoja na beki Joe Rodon kwa kiungo wa Roma Nicolo Zaniolo imekataliwa.

Paris Saint-Germain wamewapa Roma nafasi ya upendeleo kumsajili Georginio Wijnaldum, baada ya Roma kufanikiwa kukamilisha Usajili Paulo Dybala kutoka Juventus kwa uhamisho huru.

Manchester United na Chelsea wanachuana kuwania saini ya beki mahiri wa Bayern Munich Benjamin Pavard.

Juventus wanazungumza na Aaron Ramsey kuhusu kusitisha mkataba wake mapema mjini Turin. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 umebakiza mwaka mmoja na ameondolewa kwenye kikosi kinacho jiandaa na msimu mpya.

Arsenal wanajiandaa kumnunua kiungo wa Juventus, Arthur Melo kwa kumjumuisha mchezaji pamoja na pesa. The Gunners walijaribu kumsajili Mbrazil huyo mwezi Januari na sasa wamepanga kumuuza Lucas Torreira ili kumsajili kiungo huyo.

Borussia Dortmund wanafikiria kumnunua Luis Suarez mwenye umri wa miaka 35 ambaye ni mchezaji huru baada ya Mshambuliaji wao Sebastien Haller kugundulika kuwa na tezi dume.

AC Milan wanafikiria kuwanunua wachezaji wanne wa Tottenham. Mazungumzo yanaendelea kwa ajili ya kuwanunua Japhet Tanganga na Pape Matar Sarr (aliye kwa mkopo) huku mabingwa hao wa Serie A pia wakiwa na nia ya kuwanunua Tanguy Ndombele na Sergio Reguilon.

Post a Comment

0 Comments