Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Usajili: Man Utd wanafanyia kazi ombi la Ronaldo; Chelsea wahamia kwa Serge Gnabry

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Mtendaji mkuu wa Manchester United Richard Arnold anajaribu kumshawishi Cristiano Ronaldo kuondoa ombi lake la kutaka kuondoka Old Trafford.

Arnold amesafiri kwa ndege kuelekea Barcelona pamoja na mkurugenzi wa kandanda John Murtough kujaribu kufufua dili la kumsajili kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong - hatua ambayo imekwama kwa takriban wiki moja iliyopita.

United wanaweza kumgeukia Youri Tielemans wa Leicester au Ruben Neves wa Wolves iwapo hawataweza kumpata De Jong.

Chelsea wako tayari kuhama kutoka kwa Raphinha, ambaye anaelekea kujiunga na Barcelona baada ya masharti kuafikiwa na Leeds, na wanamtaka winga wa Bayern Munich Serge Gnabry.

Arsenal wametoa ofa ya pauni milioni 6 kwa Benfica kwa beki wao wa kushoto Alex Grimaldo, 26, ambaye anaingia mwaka wa mwisho kwenye mkataba wake.

AC Milan wana matumaini ya kumpata winga wa Morocco Hakim Ziyech, huku Chelsea wapo tayari kumuuza kwa uhamisho wa kudumu.

Declan Rice 'amekubaliana' na West Ham kusalia kwa msimu mmoja zaidi. Chelsea, Manchester United na Manchester City zote zinahusishwa na nyota huyo wa Uingereza.

Newcastle wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Espanyol Raul de Tomas, mchezaji huyo hapo awali alikuwa akiwindwa na Arsenal na Juventus.

Brentford wapo katika nafasi nzuri ya kumsaini golikipa kipa Thomas Strakosh ambaye anahitajika pia na Manchester United.

Mshambuliaji wa Real Madrid Rodrygo Goes amethibitisha kwamba hivi karibuni atatia saini ili kuendelea kusalia Santiago Bernabeu.

Sevilla wana nia ya kumsajili beki wa pembeni wa Tottenham, Sergio Reguilon, ambaye hakusafiri na kikosi cha kwanza kwa ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini Korea Kusini.

Liverpool wako tayari kuchuana na Manchester City kuwania saini ya kiungo Mreno Matheus Nunes. Mawasiliano yamefanywa na wawakilishi wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 23, ambae anaweza kupatikana kwa €40m.

Wolves wamekataa ofa kutoka kwa Everton kwajili ya Morgan Gibbs-White kwa sababu ofa hiyo ipo chini ya £30m ambayo ndio thamani ya mchezaji huyo. The Toffees pia wanavutiwa na kiungo wa Chelsea Conor Gallagher.

Alexis Sanchez yuko kwenye mazungumzo na Inter ili kusitisha mkataba wake baada ya Kocha Simone Inzaghi kumwambia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kwamba hayuko katika mipango yake.

Klabu za Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid zipo tayari kupambana kuwania saini ya mshambuliaji chipukizi wa Albacete Dani Gonzalez.

Post a Comment

0 Comments