Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za usajili: Bayern Munich wamgeukia Kane; Chelsea waachana na Ronaldo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Bayern Munich wapo tayari kumnunua mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane iwapo wataamua kumuuza mshambuliaji wao tegemeo Robert Lewandowski anaye takiwa na FC Barcelona katika msimu huu wa majira ya joto.


Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland ameweka wazi nia yake ya kutaka kuondoka Allianz Arena na kuelekea Barcelona. Hata hivyo, matatizo ya kiuchumi yanayo wakabili Barcelona yanaweza sababisha wasiweze kumnunua, huku Chelsea na PSG zikiwa tayari kumchukua.

Chelsea imeachana na mpango wake wa kumfuatilia Cristiano Ronaldo baada ya Thomas Tuchel kuweka wazi kwa uongozi wa The Blues kwamba hayuko tayari kumjumuisha nyota huyo wa Ureno katika kikosi chake. Wakati huohuo, winga wa Manchester CityRaheem Sterling anaweza kutambulishwa kama mchezaji wa Chelsea leo baada ya kufaulu vipimo vya afya.

Manchester United wanaweza kumaliza dirisha la usajili bila kiungo mpya wa ulinzi huku wakilenga kukamilisha usajili wa Frenkie de Jong na Christian Eriksen

Arsenal wanajiandaa kuwasilisha ofa kwa ajili ya kumnunua beki wa kushoto wa Benfica Alex Grimaldo, huku pia wakichuana na Newcastle United kwa ajili ya kumnunua kiungo wa Lyon Lucas Paqueta.

Hatimaye Barcelona wamefikia makubaliano na Leeds United kwa ajili ya uhamisho wa Raphinha, huku Ousmane Dembele akirejea kikosini baada ya kukubali kukatwa 40% ya mshahara wake.

Chelsea wameiambia Barcelona kuwa wako tayari kuachana na Cesar Azpilicueta kwa pauni milioni 7 baada ya Barca kukubaliana na nahodha huyo wa The Blues, huku Barca wakiwa na uhakika wa kumsajili Bernardo Silva kutoka Manchester City.

Tottenham  wanajiandaa kununua wachezaji wanne wakubwa baada ya kuachana na baadhi ya wachezaji wao waliokuwepo kwenye kikosi cha kwanza kilichopo ziarani nchini Korea Kusini. Sergio Reguilon anaweza kurejea Sevilla, Tanguy Ndombele anarejea kwao Ufaransa kwa mkopo, wakati Giovani Lo Celso na Harry Winks wapo sokoni.

Newcastle wameweka mezani kitita cha  €25m kwa winga wa Real Madrid Marco Asensio, ambaye anaingia mwaka wa mwisho kwenye mkataba wake. Madrid  wanahitaji ada ya angalau €30m ili kumuuza mchezaji huyo.

Magpies wanapewa nafasi kubwa ya kuwasajili Emmanuel Dennis wa Watford na Maxwel Cornet wa Burnley baada ya timu zao kushuka daraja kutoka Ligi kuu kwenda Ligi daraja la kwanza. 

Kiungo wa kati wa Arsenal Lucas Torreira amekiri kuwa amekuwa akiwasiliana na Kocha Jose Mourinho kuhusu kuhamia Roma, huku Juventus nao wakimfuatilia mchezaji huyo wa Uruguay.

Juventus wanajiandaa kutuma ofa ili kumnunua Kalidou Koulibaly huku Matthijs de Ligt akitarajiwa kujiunga na Bayern Munich au Chelsea. Maafisa kutoka Bayern wanatazamiwa kuwasili mjini Turin leo kujadili uhamisho kwajili ya Mholanzi huyo.

Manchester City wanaweza kumnunua nyota wa Uholanzi De Ligt kama Nathan Ake atajiunga na Chelsea kama inavyotazamiwa.

Liverpool wameungana na Wolves katika mbio za kumsajili kiungo wa Sporting CP Matheus Nunes, huku pia wakimfuatilia kwa karibu winga wa Athletic Club Inaki Williams.


Post a Comment

0 Comments