Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za usajili: Ronaldo Aomba Man Utd kumwachia; Juventus wanakaribia kukamilisha Usajili wa Firmino

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


Cristiano Ronaldo amedhamiria kuondoka Manchester United msimu huu wa majira ya joto baada ya kuomba kuvunja mkataba. Mkataba wake umebakiza mwaka mmoja kukamilika na una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi kwa msimu. Atletico Madrid na Bayern Munich zote zimejitoa katika kinyanganyiro cha kumuwania Ronaldo katika siku za hivi karibuni.

Juventus wanasemekana kukamilisha makubaliano ya kumsajili Roberto Firmino kutoka Liverpool, jambo ambalo litamaliza nia yao ya kuwasaka Timo Werner, Anthony Martial na Memphis Depay.

Werner na Depay wote wamepewa ofa na Newcastle United katika siku za hivi karibuni, wengine ni winga wa Arsenal Nicolas Pepe na mchezaji wa PSG Julian Draxler.

Barcelona wanaweza kutangaza kumsajili Jules Kounde leo Alhamisi baada ya kukubaliana na Sevilla kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo na kuwapiku Chelsea kwenye saini ya beki huyo. Barca pia wana uhakika wa kuwasajili Cesar Azpilicueta na Marcos Alonso kutoka Blues.

Arsenal hawana nia ya kumsajili tena kiungo wa Juventus Arthur Melo, ambaye huenda akajiunga na Valencia kwa mkopo.

Manchester City wanafuatilia mbadala wa Marc Cucurella baada ya kuchukizwa na bei ya Brighton ya £50m, na sasa wamehamishia nguvu zao kwa beki wa kushoto wa Benfica Alex Grimaldo.

Frenkie de Jong amewajulisha wachezaji wenzake wa Barcelona kwamba atasalia Camp Nou msimu huu wa majira ya joto licha ya Manchester United kukamilisha usajili wake.

Matumaini ya Leeds United na Leicester City kumsajili Charles De Ketelaere yapotea rasmi baada ya AC Milan na Club Brugge kukubaliana ada ya uhamisho kwa ajili ya fowadi huyo chipukizi.

Wakati Red Bull Salzburg ikiendelea kugoma kupokea ofa zozote za kumuuza mshambuliaji wake Benjamin Sesko msimu huu wa majira ya joto, taarifa zinadai kwamba baada ya mkataba wake kwisha mshambuliaji huyo anapendelea kujiunga na Real Madrid.

Klabu ya Everton iko tayari kutangaza kumsajili Dwight McNeil kutoka Burnley baada ya kufanyiwa vipimo vya afya Jumatano jioni.

Nottingham Forest wamefanya mazungumzo na Real Betis kuhusu uhamisho wa William Carvalho msimu wa wa majira ya joto, ingawa Los Verdiblancos wamezuia mbinu ya kumnunua Alex Moreno.

Kwa upande wa wachezaji wanaoingia, Real Betis wanaamini Arsenal watakataa kumuuza Hector Bellerin na badala yake watamwachia baada ya mkataba wake kumalizika.

Kwingineko katika safu ya ulinzi ya Arsenal, Marseille wanaendelea kuwasiliana na The Gunners kuhusu beki William Saliba, lakini anatazamiwa kusalia Emirates.

Post a Comment

0 Comments