Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za Usajili barani Ulaya: Messi Agoma Kuongeza mkataba Mpya PSG , Awataka wasubili hadi Kombe la Dunia litakapo kwisha

Lionel Messi amesema hayuko tayari kuongeza mkataba mpya na Paris Saint-Germain mbaka pale kinyanganyiro cha Kombe la Dunia litakapo fanyika mwaka huu, PSG wapo tayari kumuongezea mkataba wa mwaka mmjo mshambuliaji huyo nguli.


Arsenal wamekubaliana na Manchester City kuhusu usajili wa mchezaji Oleksandr Zinchenko kwa ada ya uhamisho wa £30m. Mazungumzo binafsi kati ya Arsenal na Zinchenko yanaendelea.

City hawana mpango wa kumuuza Bernardo Silva kwenda Barcelona katika msimu huu wa majira ya joto huku kukiwa na ripoti kwamba kama watamuuza basi si chini ya £70m.

Bayern wanaandaa ofa yenye thamani ya zaidi ya €30m kwa Mathys Tel wa Rennes, ambaye atachukua nafasi ya Lewandowski anaye timkia Barca.

Hata hivyo, Bayern kwa mara nyingine wathibitisha kwamba hakuna uwezekano wa kumnunua nyota wa Manchester United Cristiano Ronaldo, ambaye anataka kuondoka Old Trafford msimu huu wa majira ya joto.

Meneja wa United Erik ten Hag ameuambia uongozi wa klabu hiyo kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Barca Frenkie de Jong katika msimu huu wa majira ya joto.

Chelsea wanajipanga kurudisha mawazo yao kwa beki wa kati Jules Kounde huku Nathan Ake akisalia Man City.

West Ham wametuma ofa tatu zenye thamani ya pauni milioni 100 kwa jumla kwa Armando Broja wa Chelsea, Gianluca Scamacca wa Sassuolo na Amadou Onana wa Lille.

Aston Villa wameamua kumuweka sokoni Carney Chukwuemeka - ambaye ameachwa nje ya ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya - huku baadhi ya timu za Premier League zikimuhitaji na nyingine kutoka nje, zikiwemo PSG na Barcelona.

Juventus wameanza mazungumzo na Villarreal kuhusu beki wa kati Pau Torres, ambaye atachukua nafasi ya Matthijs de Ligt anayekipiga Bayern.

Wakati huo huo, Nyambizi wa Njano (Villarreal) wamefanya mawasiliano na mshambuliaji wa zamani wa Man Utd Edinson Cavani juu ya uwezekano wa uhamisho huru.

Chelsea imemsajili mshambuliaji Omari Hutchinson 18, kutoka kwa wapinzani wao Arsenal. Atajiunga na kikosi cha vijana.

Beki Calvin Bassey anakaribia kuondoka Rangers na kujiunga na Ajax kwa mkataba wa kudumu. Miamba hao wa Uholanzi pia wanakaribia kukamilisha uhamisho wa kudumu wa mshambuliaji wa RB Leipzig Brian Brobbey, licha ya mshambuliaji huyo kutakiwa na Man Utd.

Post a Comment

0 Comments