Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za usajili: Arsenal Wampa Saka Mkataba mpya; Chelsea wachukizwa na Mpango wa Barcelona

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Arsenal imempa nyota wake Bukayo Saka mkataba mpya wa muda mrefu ambao utamfanya kulipwa mshahara mara mbili ya mshahara anaolipwa sasa Emirates ili kuzuia nia ya Manchester City kutaka kumsajili.


Chelsea wamempa Jules Kounde mkataba wa miaka mitano. Hata hivyo, Barcelona wamesalia katika kumsaka beki huyo wa Sevilla na inasemekana wamefikia makubaliano kimsingi kuhusu uhamisho huo.

Meneja wa The Blues Thomas Tuchel amedokeza kuwa hajafurahishwa na kitendo cha Barca kutaka kumsajili Cesar Azpilicueta, ambaye bado amebakiza mwaka mmoja kumalizia mkataba wake Stamford Bridge.

Real Madrid walikuwa na nia ya kumsajili Gabriel Jesus kabla ya Mbrazil huyo kuchagua kujiunga na Arsenal.

Los Blancos pia wamekataa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Inter Edin Dzeko kwa sababu ya umri wake.

Newcastle wanahusishwa na kutaka kumnunua fowadi wa Barcelona Memphis Depay, ambaye ahitajiki tena Camp Nou msimu huu.

Mshambuliaji Antony  anatarajiwa kusalia ndani ya klabu ya Ajax msimu huu wa majira ya joto, kulingana na maelezo ya meneja Alfred Schreuder licha ya Manchester United kumuhitaji sana mchezaji huyo.

AC Milan hawapo tayari kulipa kiasi cha euro milioni €35m  kwa ajili ya mchezaji Charles de Ketelaere wa Club Brugge na sasa ni rasmi wameamua kujitoa kwenye dili hilo ambalo Leeds wao wameongeza ofa yao hadi €40m.

Sadio Mane ameelezea kuhama kwake kutoka Liverpool kwenda Bayern Munich kama "Ni uamuzi bora zaidi ambao nimefanya katika maisha yangu ya soka".

Georginio Wijnaldum yuko huru kuondoka Paris Saint-Germain msimu huu anatazamwa na Roma, ambayo inajiandaa kutuma maombi ya kumsajili Mholanzi huyo kwa mkopo.

Post a Comment

0 Comments