Ticker

6/recent/ticker-posts

TEN HAG AMNASA LISANDRO MARTINEZ KWA £46.5M.

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapaManchester United wanakaribia kumsajili Lisandro Martinez kwa pauni milioni 46.5 ($55m). Mazungumzo na Ajax sasa yako katika hatua za mwisho.

United ilijiweka kwenye nafasi nzuri kwa Martinez baada ya wapinzani wao, Arsenal, kurudi nyuma kwa imani kwamba mchezaji huyo alipendelea kuhamia Old Trafford.

Ajax walihofia kumuuza - wakikataa dau la awali la karibu £40m ($47m). Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina aliweka wazi kuwa anataka kuhamia Premier League na kuungana na Ten Hag, ambaye alikuwa meneja wake na mabingwa hao wa Uholanzi(Ajax).

United walisubiri kufikisha nia yao ya kumnunua Martinez lakini walijua kuwa ada ya kati ya £45-50m ingetosha kupata mkataba baada ya kuona ofa za chini kutoka kwa Arsenal zimekataliwa.

Nia ya mchezaji huyo kuungana na Ten Hag pale Old Trafford. Na huu utakuwa usajili wa pili kwa meneja Erick Ten Hag.

Post a Comment

0 Comments