Ticker

6/recent/ticker-posts

Teknolojia Mpya Kuwekwa Ndani ya Mpira Kubaini Offside

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Teknolojia Mpya Kuwekwa Ndani ya Mpira Kubaini Offside

Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi wa FIFA, Pierluigi Collina

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetambulisha ujio wa teknolojia mpya itakayotambua matukio ya kuotea kwa wachezaji “Offside” itakayoanza kutumika kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Akizungumzia ujio wa teknolojia, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi wa FIFA, Pierluigi Collina amesema teknolojia hiyo iliyopewa jina la (Semi-automated offside technology – SAOT) itakuwa mwarobaini wa changamoto na malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa waamuzi.

Teknolojia hiyo itakavyofanya kazi ni kama ifuatavyo;

Teknolojia itaendelea kusaidia kurahisisha matukio tata kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar

Kutakuwa na kamera 12 zilizofungwa juu ya Uwanja zitakazokuwa zikifuatilia maeneo 29 yanayotoa data kwenye mwili wa mchezaji kila baada ya sekunde 50 kwenye mchezo ikiwemo miguu na mikono.

Kikisio (sensor) cha kutambua ‘offside’ kitawekwa ndani ya mpira na kitatuma data mara  500 ndani ya sekunde moja, na iwapo itabainika kuna offside kitatoa mlio maalum kumpa taarifa mwamuzi.

Teknolojia hiyo itakuwa ikituma taarifa kwenda chumba cha VAR ambako kutakuwa na waamuzi wengine na endapo kama kuna tukio la ‘offside’ kwa mchezaji, watalazimika kuangalia kujiridhisha.

Teknolojia hii itaanza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia la nchini Qatar 2022

FIFA imesema teknolojia hiyo imeshafanyiwa majaribio miezi saba iliyopita katika mashindano mawili makubwa duniani na kutoa majibu chanya, hivyo ni wasaa sasa wa kuitumia katika Fainali ya Kombe la Dunia.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi


Post a Comment

0 Comments