Ticker

6/recent/ticker-posts

Singida yashusha Wabrazili Wawili na Kuwaficha

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


TIMU ya Singida Big Stars Imefanikiwa kupata saini ya Wabrazili, Bruno Gomez na Dario Fredrico.

Licha ya Nyota hao kufichwa na timu hiyo laniki taarifa za kina ambazo mdodosaji Imezipata ni kwamba wachezaji hao wameanza mazoezi rasmi huku wakiwa chini ya uangalizi maalumu na baadhi ya viongozi hawataki wapigwe picha hadi watakapotambulishwa rasmi.

Gomes, Fredrico ni viungo washambuliaji wapo jijini Arusha kwenye kambi ya timu hiyo inayojiandaa na maandalizi ya msimu (pre season) na wameanza kuwavutia mabosi wao.

“Ni wachezaji wazuri na mazoezini wameonyesha wana vitu japokuwa viongozi wamefanya siri, ila muda wowote watawatambulisha akiwemo pia na Pascal (Wawa).” kilisema chanzo hicho.

Singida iliyo chini ya Mholanzi, Hans van der Pluijm na msaidizi wake Mganda, Mathias Lule inajifua jijini Arusha tangu Julai 22 na baada ya hapo itakwenda Singida ambako ndio makao yake makuu kujiandaa na Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 17.

Hadi sasa Singida imenasa saini ya mastaa kadhaa wakiwemo, Aziz Andambwile (Mbeya City), Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar), Benedict Haule (Azam FC) na Metacha Mnata (Polisi Tanzania). Wengine ni, Abdulmajid Mangalo (Biashara United), Said Ndemla (Mtibwa Sugar), Pascal Wawa (Simba) na Deus Kaseke, Yassin Mustapha, Paul Godfrey ‘Boxer’ wote kutoka (Yanga).

Post a Comment

0 Comments