Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba wakutana kumaliza tofauti zao

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Viongozi wa Simba wakutana na kumaliza tofauti zao

BAADA ya kupoteza ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu mbele ya Yanga, viongozi na wadau wa Simba wamekutana na kumaliza tofauti zao na kujipanga upya na kuweka mikakati ya msimu ujao.

Viongozi hao wanadaiwa kwamba, hawakuwa kitu kimoja kwa msimu huu na kusababisha timu hiyo kushindwa kufikia malengo ya kutetea taji la Ligi Kuu na lile la FA.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya mmoja wa kigogo ambaye hakutaka jina lake kutajwa, alisema kikao hicho kiliongozwa na Rais wa heshima wa timu hiyo, Mohammed Dewji kwa kuzungumza mambo mbalimbali ikiwemo mikakati ya msimu ujao pamoja na kumaliza tofauti baina yao.

Alisema katika mikakati hiyo walijadili na kutathimini kikosi chao na jinsi gani ya usajili wa wachezaji wapya waliosajiliwa, lakini pia timu hiyo kwenda nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

“Tulikutana kwa ajili ya kumaliza sintofahamu iliyokuwepo kwa msimu huu baada ya kushindwa kufanya vizuri na tumeweka tofaauti zetu pembeni na sasa tuna ungana upya kwa ajili ya msimu ujao na tayari tumeshaweka mikakati yetu,” alisema kigogo huyo.

Baadae mmoja wa wajumbe na wadau wa wakubwa wa Simba, Crescentius Magori aliandika ujumbe mfupi kupitia ukurasa wake wa instagram akisema: "Katika umoja wetu (kama timu) tunajenga nyumba moja, kwa sababu katika Muungano kuna nguvu ya pamoja, mazuri yanakuja.”


Post a Comment

0 Comments