Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Yaanza Mazoezi Rasmi Nchini Misri

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Simba Yaanza Mazoezi Rasmi Nchini Misri

Kikosi cha Simba kimetua jananchini Misri na wachezaji wakafanya mazoezi kwa awamu ya kwanza wakiwa katika ardhi hiyo kama maandalizi ya msimu ujao, huku kocha wa timu hiyo, Zoran Maki akichekelea usajili uliofanywa akisema; ‘Wameumia’.

Zoran aliyeajiriwa hivi karibuni kwa mkataba wa mwaka mmoja, alisema usajili uliofanywa hadi sasa unampa picha atakuwa na timu kali ambayo itasumbua kwenye msimu ujao wa mashindano kuanzia Ligi Kuu Bara, ASFC hadi michuano ya kimataifa.

Akizungumza Zoran alisema amemfuatilia Moses Phiri anayetokea Zambia na kusema ni moja ya wachezaji wazuri mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi za kufunga, kufunga mwenyewe na ndani ya msimu mmoja anaweza kufunga si chini ya mabao kumi.

Alisema uwepo wa Phiri katika kikosi chake utampa nafasi ya kumtumia kutokea pembeni kushoto au kulia, nyuma ya mshambuliaji au hata kwenye kiungo na kote anaweza kufanya vizuri kutokana na uwezo wake.

“Nimefuatilia Ligi Kuu ya Ghana nimemuona vizuri huyo Augustine Okrah ni aina ya mchezaji mwenye kipaji si katika kushambulia tu bali anawasumbua hata mabeki wa timu pinzani,” alisema Zoran na kuongeza;

“Uwepo wa Okrah katika kikosi chetu na kama atacheza kwenye kiwango nilichomuona akiwa ndani ya timu yetu nina imani utakuwa moja ya usajili mzuri kutokana na uwezo alionao.

Post a Comment

0 Comments