Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba kuweka kambi Misri kwa Maandalizi ya msimu Ujao

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 KIKOSI cha Simba kinatarajia kuingia kambini Jumanne tayari kuanza maandalizi ya safari ya kuelekea Misri ili kujiwinda kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa watakayoshiriki.

Taarifa kutoka Simba inasema kikosi hicho kitaondoka nchini kati ya Julai 14 na 15, mwaka huu na kitaungana na Kocha Mkuu mpya, Zaron Manojlovic jijini Cairo.

Chanzo cha kuaminika kinadai katika maandalizi ya safari hiyo, baadhi ya wachezaji jana walienda kufanya vipimo mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili.

"Msimu huu ulioisha hatukufikia malengo, kuanzia ligi ya ndani na michuano ya kimataifa, tutaingia kambini mapema na baadhi ya wachezaji watakutana hapa nchini na wengine wataungana na wenzao baada ya kufika Misri," kilisema chanzo chetu.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema Zaron ataungana na timu yake moja kwa moja katika nchi watakayokwenda kuweka kambi.

“Wachezaji watakutana Dar es Salaam na kuhusu usajili umeenda vizuri, tumekamilisha kusuka kikosi , wachezaji tuliowahitaji wapo kwenye makaratasi yetu, muda si mrefu tutaanza kushusha vyuma,” alisema Ahmed.


Post a Comment

0 Comments