Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Kumrudisha Luis Miquissone

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Simba Kumrudisha Luis Miquissone 

KLABU ya Simba, ipo katika mchakato wa kumrudisha kikosini kiungo mshambuliaji raia wa Msumbiji, Luís Jose Miquissone kutoka Al Ahly ya Misri.

Miquissone anarejea baada ya kupata wakati mgumu ndani ya Al Ahly tangu alipojiunga na timu hiyo Agosti 26, 2021 akisaini mkataba wa miaka minne akitokea Simba.

Baada ya Al Ahly kuachana na Kocha Mkuu, Pitso Mosimane na nafasi yake kuchukuliwa na Ricardo Soares, imeripotiwa kwamba Luis hayupo tena katika mipango ya kocha huyo.

Kwa mujibu wa mabosi wa Al Ahly, kiungo huyo tangu ametua hapo, hajaonesha kiwango kizuri, hivyo Soares, baada ya kuangalia tathmini ya kikosi chake, amemuondoa Luis kwenye mipango yake. Kwa sasa Al Ahly inaangalia namna ya kusajili mbadala wa nafasi yake.

Uamuzi uliochukuliwa ni kumuachia Luis aondoke kikosini hapo iwe kwa mkopo au kuuzwa moja kwa moja, kwa sasa anasubiriwa Miquissone na wawakilishi wake kujadili hilo kabla ya kufanyika uamuzi.

Wakati Luis anauzwa, uongozi wa Simba ulisema kwamba, walikubaliana na Al Ahly kwamba mchezaji huyo endapo akiondoka Al Ahly, Simba ina nafasi ya kwanza kumrudisha hapa nchini kuliko timu yoyote ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments