Ticker

6/recent/ticker-posts

Simba Ilivyompa Denis Nkane Mkataba Yanga..Nkane Na Johari Ndani Ya Penzi Mbashara

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Simba Ilivyompa Denis Nkane Mkataba Yanga..Nkane Na Johari Ndani Ya Penzi Mbashara

 Licha ya rekodi ya kucheza miezi sita tu na kutwaa mataji mawili akiwa na Yanga, winga Denis Nkane ni mmoja wa wachezaji wenye bahati.

Mbali na rekodi ya kutwaa mataji mawili ndani ya miezi sita, Nkane amecheza Kombe la Shirikisho Afrika akiwa na Biashara United na kufunga mabao mawili kwenye mashindano hayo.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi

Unataka kufahanu ni kwanini? Iko hivi; kinda huyo aliyepandishwa kutoka kikosi cha vijana cha Kagera Sugar na kupandishwa Ligi Kuu ametwaa taji la Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho akicheza dakika 1087, kufunga mabao matatu na kadi mbili za njano hana kadi nyekundu.


Mchezaji huyo ameifungia Yanga bao moja kwenye ligi na Biashara mawili na pasi za mwisho mbili (asisti).


Nkane amefunguka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na rekodi aliyoitengeneza msimu uliopita ambao amekiri kuwa ulikuwa bora sana kwake.


MSIMU WA KIBABE


Anasema: “(Uliopita ulikuwa) ni msimu bora na mzuri kwangu pamoja na changamoto mbalimbali nilizopitia, lakini najivunia kutwaa mataji mawili na kucheza timu ya ndoto zangu sambamba na kushiriki mashindano makubwa.”


Anasema akiwa Biashara United walicheza Kombe la Shirikisho Afrika akifunga bao moja na pasi moja iliyozaa bao lakini ukata uliwakwamisha kumaliza mashindano, kwani walitakiwa kwenda kumalizana na Al Ahly Tripoli ya Libya, lakini hawakufanya hivyo.


AZAM, CAMBIASO


Safari yake ya soka ilimpitisha Azam FC na Cambiaso na hapa anasema: “Safari yangu ya soka imeanzia mtaani, lakini nilipata bahati ya kupita Azam FC kufanya majaribio wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, lakini sikuwa na bahati, sikufanikiwa.”


Baada ya hapo alijaribu Cambiaso ambapo majaribio ya mchujo alipita awamu ya kwanza na kucheza kidogo awamu nyingine mchujo ulinipita akaondolewa.


Nkane anasema baada ya hapo alicheza mchezo wa kirafiki na timu ya mtaani kwake Uwanja wa Karume na kuonwa na kiongozi wa timu ya Njombe aliyempa nafasi kuonyesha kipaji timu hiyo iliyokuwa inashiriki Ligi Daraja la Tatu na ndio ukawa mwanzo wake wa kuonekana hadi Biashara United timu ya vijana.


SIMBA YAMPA ULAJI YANGA


Nkane anasema kufikia alipo, kapambana sana. “Nikiwa timu ya vijana ya Biashara United nilipandishwa timu ya wakubwa kocha Francis Baraza ndiye aliyeona kipaji changu,” anasema.


“Nakumbuka siku Biashara inacheza na Namungo kocha aliniita na kuniuliza kama najiamini na naweza kucheza jibu lilikuwa najiamini na naweza nikijua anataka kunipanga mechi hiyo.”


Anasema aliulizwa hivyo, lakini hakupangwa kwenye mchezo wa siku hiyo, ila mechi iliyofuata dhidi ya Simba alijiona kikosi cha kwanza mchezo anaodai baadhi ya viongozi hawakufurahishwa kupangwa kwake.


“Kabla ya mechi nahodha wangu kipindi hicho Biashara, Abdulmajid Mangaro alikaa nami na kuniambia nisiwe na presha mechi za Simba na Yanga ni za kawaida kuliko nyingine kinachowapa presha wachezaji ni wingi wa mashabiki, nililipokea hilo na kuingia nikiwa na ujasiri. Nakumbuka tulifungwa bao 1-0 Simba ikiwa na kina Clatous Chama,” anasema na kuwa pamoja na kufungwa kocha alimpongeza na ukawa mwanzo wa kumuamini.


OFA YA YANGA


Akiizungumza Yanga ilivyomnasa, Nkane ansema: “Nakumbuka baada ya mchezo wa mzunguko wa pili na Coastal Union nilipokea simu kutoka kwa kiongozi mkubwa wa Yanga ambaye alionyesha kuvutiwa na uwezo wangu siku hiyo nilikuwa na furaha kubwa sana.”


“Washauri wangu hawakutaka niondoke Biashara United wakiamini kuwa umri wangu ni mdogo natakiwa kukomaa zaidi kwa kuongeza misimu miwili kucheza ili kujihakikishia mazingira mazuri, ubora wa kipaji na ukomavu lakini hilo sikulielewa kwani niliona ndoto yangu inaenda kutimia.”


BANGALA BALAA


Kuhusu kiungo wa Yanga, Yanick Bangala anamzungumzia akisema: “Nimecheza nusu msimu, lakini nimeshuhudia kipaji kikubwa ambacho sikutarajia kukutana nacho kwenye ligi. Yanick Bangala ni mchezaji bora kastahili ni muhimu sana kwenye kikosi cha timu yetu.”


“Hana mambo mengi ni mchezaji ambaye anaamini kwenye kipaji na mazoezi muda wake wa mapumziko yeye ni kulala na kuchezea simu. Ni moja ya wachezaji ambaye anatambua muda wa kupumzisha mwili na mazoezi.”


AMTAMANI JOHARI


Ukimuuliza ni jambo gani angefanya kama asingecheza soka, Nkane anasema: “Mbali na kuibukia kwenye soka malengo yangu makubwa yalikuwa kuingia kwenye filamu, lakini nilishindwa na kujikuta naangukia kwenye soka, sijutii hili ni mipango ya Mungu.”


“Nilichofanya kwenye soka naamini ningekuwa upande wa filamu pia kungekuwa na kitu nimekiongeza. Mwanadada Blandina Chagula ‘Johari’ ndiye msanii aliyekuwa ananivutia zaidi kutokana na uigizaji pamoja na ndoto yangu kukatika natamani kuonana naye, naamini kuna kitu nitamshirikisha.”


MIEZI MINANE BILA BAO


Nkane ambaye alisajiliwa Yanga dirisha dogo la usajili mara ya mwisho kufunga bao ilikuwa Desemba 21 akiwa na Biashara dhidi ya Namungo Uwanja wa Ilulu, anasema alipitia wakati mgumu.


Baada ya kufunga mwezi huo Nkane alipata nafasi ya kuifungia Yanga bao lake la kwanza Juni 29 akiwatungua Mtibwa Sugar bao 1-0, kisha Coastal Union katika fainali ya ASFC.

Post a Comment

0 Comments