Ticker

6/recent/ticker-posts

Serge Gnabry asaini mkataba mpya Bayern Munich

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Serge Gnabry asaini mkataba mpya Bayern Munich

Bayern Munich wamethibitisha kwamba winga Serge Gnabry amesaini mkataba mpya wa miaka minne Allianz Arena.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa ameingia miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake wa awali na alipenda kuondoka mapema msimu huu wa majira ya joto, huku Arsenal na Chelsea wakimfuatilia Gnabry kwa Ukaribu.

Sasa, sakata hilo limefika tamati baada ya Bayern kumpa Gnabry kandarasi mpya hadi 2026.

"Nilifikiria sana juu ya kile ninachohitaji kama mchezaji katika miaka ijayo, na nikafikia hitimisho kwamba nataka kubaki FC Bayern, kushinda kila kitu nikiwa hapa na kujifunza vitu vingi zaidi - hasa kusherehekea taji lingine la Ligi ya Mabingwa, lakini wakati huu na mashabiki wetu," Gnabry alisema.

"Hii ni maalum kwangu kwa sababu ninapata kucheza hapa na marafiki zangu katika kiwango cha juu zaidi. Kwa hakika nisingejisikia sawa nikiwa na klabu tofauti. Nataka kupata wakati mzuri zaidi hapa - na hakuna mahala pengine."

Rais wa klabu Herbert Hainer aliongeza: "Ni ishara nyingine kali kwamba mchezaji kama Serge Gnabry anauona mustakabali wake ndani ya FC Bayern.

"Ameshinda kila kitu akiwa hapa na anatambulika na klabu kiasi kwamba anataka kusaidia kuandika  historia zaidi klabuni. Anapokuwa na mpira, anavutia kutazama. Pamoja naye, Sadio Mane, Thomas Müller, Kingsley Coman, Leroy Sané na Jamal Musiala, FC Bayern wana machaguo bora zaidi ya mawinga wa pembeni ambao ni bora katika soka la Ulaya."

Taarifa za Gnabry Kusaini mkataba mpya zilitoka dakika chache baada ya Hainer kuthibitisha kwamba makubaliano yamefikiwa ya kumuuza mshambuliaji wao nyota Robert Lewandowski kwenda Barcelona.

Post a Comment

0 Comments