Ticker

6/recent/ticker-posts

Sababu ya Cristiano Ronaldo Kutaka Kuondoka Manchester United

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  • Wakala wa Cristiano Ronaldo amekuwa akitumia mshahara mdogo kujaribu kuvizia vilabu vikuu kumsajili. 
  • Nyota huyo Mreno bado hajarejelea kufanya mazoezi na Manchester United, huku msimu mpya wa ligi ukikaribia kuanza. 
  • Vilabu kadhaa vikuu vikiwemo Chelsea na Bayern Munich tayari vimejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kupata saini ya nguli huyo mwenye umri wa miaka 37. 
  • Duru pia karibu na Ronaldo imefichua kuwa anataka kuondoka United na kuelekea kwenye klabu ambayo hatakuwa tegemeo kubwa. 


Wakala wa Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes anaripotiwa kwamba amekuwa akitumia mshahara wa chini kujaribu kuvishawishi vilabu vikubwa kumsajili nguli huyo. 

Wiki tatu baada ya Ronaldo kutangaza nia yake ya kutaka kugura Old Trafford, bado nyota huyo Mreno hajapata ofa ya klabu yoyote kumsajili huku muda ukiendelea kuyoyoma. 

Inasemekana Ronaldo anapendelea klabu inayocheza Ligi ya Mabingwa, lakini hadi sasa, hajabahatika kuipata.

Ronaldo, 37, bado hajarejelea kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Manchester United ambao tayari wameshiirki mechi tatu ya kirafiki. 

Bayern Munich, Paris Saint Germain na Chelsea tayari wamefutilia mbali uwezekano wa kumsajili Cristiano. 

Atletico Madrid ndio klabu ya sasa inayoshirikishwa na Ronaldo, japo iliripotiwa na Sport kuwa miamba hao La Liga hawana uwezo wa kumlipa mshahara mkubwa. 

Kama sehemu ya mpango wake wa biashara, wakala mkuu ameambia vilabu kwamba mteja wake yuko tayari kukatwa 30% ya mshahara, ikimaanisha kuwa angelipwa pauni 300,000 kwa wiki. 

Lakini Ben Jacobs anafunguka zaidi kuwa kando na Ligi ya Mabingwa, kuna sababu nyingine inayochochea hatua ya Ronaldo kutaka kuondoka Old Trafford. 

Alisema kuwa duru karibu na Ronaldo imefichua kwamba anataka kuondoka United na kuelekea kwenye klabu ambayo hatakuwa tegemeo kubwa 

Ronaldo pia ana nia ya kujiunga na klabu ambayo hatakuwa mzigo katika mafanikio yao, hasusan kutokana na umri wake na Kombe la Dunia ijayo. 

Akiwa United msimu uliopita, alikuwa kitovu cha timu hiyo, akiibuka mfungaji bora kutokana na mabao yake 22, ambayo baadhi yake yalionekana kuwa muhimu kwa timu yake.


Post a Comment

0 Comments