Ticker

6/recent/ticker-posts

Romelu Lukaku Arejea Inter Milan Kwa Mkopo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Romelu Lukaku Arejea Inter Milan Kwa Mkopo 


MSHAMBULIAJI raia wa Ubelgiji, Romelu Lukaku, 29, amerejea Inter Milan kwa mkopo, Akitokea chelsea takriban mwaka mmoja tangu Asajiliwe Stamford Bridge.

Chelsea waliweka mezani kima cha Sh13.7 bilioni kwa ajili ya Lukaku mwishoni mwa msimu wa 2020-21. Hata hivyo, nyota huyo wa zamani wa Everton na Manchester United alisema “hafurahii maisha ndani ya Stamford Bridge na kwamba yalikuwa matamanio yake kurejea Italia.”

Inter wamekubali kuweka mezani kima cha Sh1.02 bilioni kufanikisha uhamisho wa Lukaku aliyewasaidia kutia kapuni taji la Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mnamo 2020-21.

Japo Chelsea hawakumtumia Lukaku mara nyingi msimu wa 2021-22, mfungaji huyo alipachika wavuni mabao 15 katika mashindano yote.

Lukaku alikuwa radhi kupunguziwa mshahara wake ili kufanikisha uhamisho wake kwenda Inter kwa mkataba wa kudumu, hali tete ya kifedha kambini mwa Inter isingewezesha kumudu mshahara wa mshambuliaji huyo.

“Nimerudi nyumbani. Nina furaha tele kuingia upya katika sajili ya Inter,” alisema Lukaku baada ya kurejea.

Lukaku aliagana na Chelsea mnamo 2014 na kutimkia Everton baada ya kusajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano uliogharimu Sh4 bilioni.

Hata hivyo, alitatizwa na visa vingi vya majeraha katika awamu ya pili ya kuhudumu kwake kambini mwa Chelsea huku akifungia kikosi hicho cha kocha Thomas Tuchel mabao matatu pekee katika mechi 15 za mwisho kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2021-22.

Chelsea walikamilisha kampeni za EPL katika nafasi ya tatu huku Liverpool ikiwafunga kwenye fainali ya Kombe la FA na League Cup kupitia mikwaju ya penalti.

Kwa upande wao, Inter waliambulia nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali la Serie A mnamo 2021-22 baada ya kupigwa kumbo na AC Milan waliotawazwa mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10.

Kurejea kwa Lukaku Inter ni afueni tele kwa kikosi hicho kinachohusishwa pia na uwezekano wa kumsajili fowadi matata wa Juventus, Paulo Dybala.

Mkataba wa sasa kati ya Juventus na Dybala ambaye ni raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 28, utatamatika rasmi mwishoni mwa Juni 2022.

Post a Comment

0 Comments