Ticker

6/recent/ticker-posts

Riyad Mahrez aongeza mkataba kuendelea kuitumikia Man City hadi 2025

Klabu ya Manchester City imetangaza kuwa Riyad Mahrez ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi 2025.

Mahrez amesalia na mabingwa hao wa Premier League baada ya washambuliaji Raheem Sterling na Gabriel Jesus kutimka katika dirisha hili la uhamisho .


City wametangaza siku ya Ijumaa kwamba Mahrez ameongeza muda kuendelea kusalia katika Uwanja wa Etihad, huku mkataba wake wa awali unatarajiwa kamilika 2023.

"Nina furaha sana kusaini mkataba mpya," Mahrez aliambia chaneli ya klabu ya City. "Nimefurahia kila dakika na muda wangu nikiwa hapa. Ni furaha kuwa sehemu ya klabu kubwa kama hii.

"Kutusaidia kufikia mafanikio ambayo tumefurahia katika misimu minne iliyopita imekuwa jambo lisilosahaulika na kutufanya sote kuwa na hamu ya kutafuta kufanikiwa zaidi.

"Pia napenda kumshukuru Pep, Txiki na benchi la Ufundi, kwa jinsi walivyonisaidia kujiendeleza kama mchezaji na kunisukuma kuendelea kuimarika.

"Sasa nataka kujaribu kutoa mchango wangu katika kuisaidia timu kuwa na mafanikio msimu ujao na zaidi."

Post a Comment

0 Comments