Ticker

6/recent/ticker-posts

Richarlison Atua Totenham Hotspurs kwa mkataba wa miaka mitano

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Totenham Hotspurs Wainasa saini ya Richarlison 

KLABU ya soka ya Totenham Hotspurs imefanikiwa kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Everton na timu ya Taifa ya Brazil Richarlison kwa ada ya paundi milioni 50.

 Kwa mujibu wa mwandishi wa Habari za michezo anayeshughulika na taarifa za usajili barani humo, Fabrizio Romano amethibitisha kuwa Totenham wamefanikiwa kutoa kitita hicho huku Richarlison akifanikiwa pia kufuzu vipimo vya afya tayari kwa ajili ya kusaini kandarasi ya miaka mitano (5) ambapo mkataba wake anatarajiwa kumalizika 2027.

Richarlison kabla ya kuichezea Klabu ya Everton alipata kufanya kazi na klabu ya Watford ya Uingereza ambayo nayo imeshuka daraja msimu huu.

Kutokana na kuwa na msimu mzuri akiwa na Everton Raia huyo wa Brazil alikuwa akigombewa na vilabu kadhaa ikiwemo Chelsea Pamoja na Klabu ya Barcelona lakini ni Totenham Hotspurs ndiyo wameibuka washindi katika mbio hizo za kuinasa Saini ya Richarlison.

Aina ya uchezaji wake imekuwa ikifananishwa na ile ya mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Hispania Pamoja na vilabu vya Atletico Madrid Pamoja na Chelsea ya Uingereza, Diego Costa.

Je,Unatafuta Ajira? Bofya hapa Kutuma Maombi

Post a Comment

0 Comments