Ticker

6/recent/ticker-posts

Paul Pogba kutambulishwa Juventus Muda wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Paul Pogba kutambulishwa Juventus Muda wowote


PAUL POGBA  yupo katika hatua za mwisho kurejea Juventus kwa Uhamisho huru, akitarajiwa kufanyiwa vipimo vya Afya wiki hii.

Pogba anaondoka Manchester United kwa mara ya pili, msimu wa 2021/22 baada ya mkataba wake kwisha.

Pogba mwenye miaka 29 amegoma kuongeza mkataba mpya Old Trafford baada ya mkataba wake wa miaka sita aliosaini na Manchester United akitokea juve kwa ada ya uwamisho wa pauni milioni 89 kufika tamati.

Pogba amekubali kujiunga na Bianconeri kwa mkataba wa miaka minne, licha ya Real Madrid na Paris Saint-Germain kumuhitaji.

Makubaliano kati ya juve na pogba yemechelewa kutokana na vipengele vya haki za matangazo kwenye mkataba wake,lakini sasa mambo ni mazuri na Pogba anakaribia kujiunga Juve kwa mkataba wa miaka minne utakao mwezesha kuwa hapo mbaka mwaka 2026.

Ripoti za uhakika zinadai kwamba kuongo huyo wa zamani wa Man Utd anatarajia kutua Turin wiki hii tayari kufanyiwa vipimo vya Afya kabla ya kujiunga na timu hiyo kwa maandalizi ya msimu mpya.

Pogba Anarejea Italy kujiunga na meneja wake wa zamani Max Allegri  aliye dumunaye kwa misimu miwili kati ya msimu wa mwaka 2014 na 2016,kabla ya kutimkia Manchester United.


Post a Comment

0 Comments