Ticker

6/recent/ticker-posts

Paul Pogba anaweza kukosa Kombe la Dunia kutokana na jeraha la goti


Matumaini ya Kiungo Paul Pogba kushiriki Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar yamepata pigo kufuatia vipimo vya hivi majuzi kuhusu jeraha lake la goti.

Kiungo huyo alirejea Juventus kwa uhamisho huru akitokea Manchester United msimu huu wa majira ya joto, lakini maandalizi yake ya msimu mpya yalitatizika alipopata jeraha la goti alipokuwa mazoezini wiki iliyopita.

Baada ya vipimo vya awali, Pogba anatarajiwa kufanyiwa upasuaji nchini Marekani, ambapo Juve wapo katika ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya.

Mchezaji huyo anatarajia kukutana na wataalamu kujadili hatua bora zaidi ya matibabu huku akiwa na matumaini kwamba anaweza kurejea uwanjani kabla ya Kombe la Dunia.

Post a Comment

0 Comments