Ticker

6/recent/ticker-posts

Nyota Ya Abbas Tarimba Yaibeba Yanga SportPesa

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Nyota Ya Abbas Tarimba Yaibeba Yanga SportPesa


Mchambuzi wa Soka, Mfaume Nalinga ametoa maoni yake juu ya Mkataba ulioingia klabu ya Yanga na SportPesa huku akibainisha kuwa klabu ya Yanga haikustahili kupata dili hilo kwani haina thamani hiyo.

Amebainisha kuwa uwepo wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa ambaye ni shabiki na Mwanachama wa klabu ya Yanga Abbas Tarimba umechochea suala hilo kupelekwa kishabiki na Yanga kupata dili ambalo lina thamani kubwa kuliko thamani halisi ya klabu hiyo.

Jana klabu ya Yanga iliingia mkataba na Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa wenye thamani ya Bilioni 12.033 kwa kipindi cha miaka mitatu (3) ambao utakuwa na mchanganuo wa kuipatia klabu ya Yanga kiasi cha shilingi Bilioni 4 kila mwaka.

Post a Comment

0 Comments