Ticker

6/recent/ticker-posts

Nelson Okwa Kutua Simba Mda Wowote

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Nelson Okwa Kutua Simba Mda Wowote

KIRAKA Nasoro Kapama wa Kagera Sugar alitambulishwa jana mchana Msimbazi. Imeisha hiyo. Hadi dirisha kubwa la usajili wa Ligi Kuu Bara linafungwa Agosti 31, Simba itakuwa imesajili mashine nane mpya kama vyombo vya habari  vilivyoripoti.


Mmoja wao ni straika Mnigeria, Nelson Okwa ambaye ameliambia Mwanaspoti kwamba atatua Dar es es Salaam punde akiwa tayari kukiwasha Msimbazi kwani kwa sasa kuna ishu kidogo tu za kukamilisha.


Kumbuka kuna mashine nyingine mpya ambazo ni Moses Phiri, Habibu Kyombo, Kapama, Victor Akpan ambao wameshatangazwa. Mohamed Outtara, Cesar Manzoki, Nelson Okwa na Augustine Okrah watafuata muda wowote kuanzia leo.


Mwanaspoti limeelezwa usajili wa Okwa uliwagharimu Simba Sh140 milioni kwavile bado alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Rivers United ya Nigeria.


Alipotafutwa Okwa alisema zaidi ya asilimia 80, kila kitu amekubaliana na Simba ila kilichobakia ni mambo mawili malipo ya timu pamoja na yeye binafsi kisha atawasili nchini kukiwasha.


“Jambo jingine huku kwetu Nigeria msimu unamalizika Jumapili ya wiki hii, tunacheza mechi ya fainali kwenye shindano la ndani na baada ya hapo nitakuwa huru kuanza taratibu na kuweka mambo sawa ili kujiunga na timu yangu mpya ya Simba kikamilifu,” alisema Okwa na kuongeza;


“Kujiunga Simba inaweza kuwa wiki ijayo nitakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kwani kila kitu kimekwenda vizuri kama tulivyokubaliana na kazi imebaki tu kwao Simba.


“Nitafurahi kuja Tanzania kwa mara nyingine tena kujiunga na timu kubwa kama Simba. Nakuja kupambana ili kuisaidia timu yangu mpya kuwa na msimu mzuri zaidi ya huu uliomalizika kwani nimeambiwa wamemaliza bila ya taji kubwa la ndani.”


Mchezaji wa zamani Simba, Mussa Hassan Mgosi alisema timu hiyo inahitaji mchezaji mwenye ubunifu na uwezo wa kushambulia kama Okwa kwani anaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji wa kati au kutokea pembeni.


“Ukiangalia msimu uliopita Simba haikuwa na ubora kwenye kutengeneza nafasi za wazi za kufunga pengine ndio maana Clatous Chama alirudishwa kwenye dirisha dogo la usajili,” alisema Mgosi na kuongeza;


“Okwa anaiweza kazi hiyo na ana sifa nyingine kuwasumbua mabeki na kufunga mwenyewe ila ataongeza ushindani dhidi yake na Chama.”

Post a Comment

0 Comments