Ticker

6/recent/ticker-posts

Moses Phiri Atua Misri

NYOTA mpya wa Simba, Moses Phiri pamoja na wachezaji wengine wanne jana walikwea pipa kwenda kambini Misri na leo wataanza mazoezi sambamba na wenzao.

Mbali na Phiri aliyesajiliwa kutoka Zanaco ya Zambia, pia msafara wa jana wa Simba ni Taddeo Lwanga, Peter Banda, Henock Inonga na Nassor Kapama.

Nyota hao walikwama kuambatana na wenzao kwa sababu ya hati zao za kusafiria na sasa wanaunga na wenzao 19 waliotangulia mapema kambini mjini Ismailia kwa maandalizi ya msimu mpya chini ya Kocha Zoran Maki.

Phiri na wenzake walianza kuliamsha jana kwenye mazoezi, huku likisubiriwa kundi la mwisho la wachezaji waliopo timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa na mechi mbili za kufuzu Fainali za CAH 2023 dhidi ya Somalia.

Mzambia huyo aliyekuwa akiwindwa na Yanga kabla ya kuamua kutua Msimbazi, anasubiriwa na hamu kubwa na mashabiki wa klabu hiyo mara msimu mopya wa mashindano utakapoanza.

Simba itakayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, imejichimbia hoteli ya Mercure Ismailia Forsan Island.

Post a Comment

0 Comments