Ticker

6/recent/ticker-posts

Morrison apewa namba mpya Yanga

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

WINGA mpya wa yanga Bernard Morrison amepangua jezi za mastaa wa timu hiyo baada ya kushindwa kupata namba yake pendwa (3) kutoka kwa nahodha, Bakari Mwamnyeto.


Akiwa Simba, Morrison alikuwa anavaa namba hiyo na alitaka kuendelea nayo Yanga, lakini Mwamnyeto amegoma kuiachia na kumlazimu Morrison kumvua jezi namba 33 beki wa kushoto, David Bryson.

Baada ya kuchukua namba 33, Bryson ameshuka kwa eki Yusuph Athuman na kuchukua jezi namba 21 huku Athuman akichukua namba 14 iliyokuwa inavaliwa na Paul Godfrey ‘Boxer’ aliyetimkia Singida Big Stars (SBS).

Haikuishia hapo mshambuliaji Lazarous Kambole amepewa namba 17 iliyokuwa ikivaliwa na kiungo Balama Mapinduzi aliyemaliza mkataba, kiungo mpya Gael Bigirimana namba 27 iliyokuwa ya Deus Kaseke aliyetimkia SBS. Beki mpya wa kulia Joyce Lomalisa namba 13 iliyokuwa ya kipa Ramadhan Kabwili waliyeachana naye.

Wakati huohuo, kocha msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amefunguka kuwa wana wiki mbili ngumu kukinoa kikosi hicho kuwa cha ushindani ndani na nje.

Kaze alisema wiki hizo zinatosha kuwaweka fiti wachezaji huku akisisitiza kuwa wanahitaji ubora kwa kila mchezaji kwa sababu hakuna aliyesajiliwa kukaa benchi kwani wana mashindano mengi.

“Tuna mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam na Mapinduzi hivyo sio ratiba rahisi kwetu tunahitaji wachezaji wenye utimamu, tunaamini ndani ya wiki hizi mbili tunaweza kukamilisha mipango yetu sisi kama benchi la ufundi na kuwaachia wachezaji wafanye kazi yao,” alisema.

“Watu wengi wanaamini kuwa tumechelewa kuanza maandalizi ya msimu mpya sio kweli. Mapumziko waliyopewa wachezaji ni sahihi kutokana na kazi kubwa waliyofanya. Wamerudi kwenye majukumu sasa ni suala la kujiweka fiti na kuhakikisha wanatetea mataji yote.” alisema Kaze ambaye yupo na timu kambini Avic

Post a Comment

0 Comments