Ticker

6/recent/ticker-posts

Mohamed Salah Asaini mkataba mpya na Liverpool mbaka 2025

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Mohamed Salah Asaini mkataba mpya na Liverpool mbaka 2025


Winga wa timu ya taifa ya misri na Klabu ya liverpool mohamed salah amesaini mkataba mpya na Liverpool utakao mwezesha winga huyo kusalia na majogoo hao mbaka juni mwaka 2025.

Salah hapo awali aligoma kusaini mkataba mpya mbaka pale liverpool watakapo mboreshea maslahi yake na kwa kuzingatia hilo liverpool wamekubali kumwongezea nyongeza ya mshahara aliyokuwa anataka. 

Baada ya kusaini mkataba mpya nyota huyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii aliandika ujumbe mfupi kuwa “Najiskia mwenye furaha kushinda makombe yote nikiwa na Liverpool. Ni siku ya furaha kwa kila mmoja wetu. Hatimaye kila kitu kipo sawa”, Mo Salah . 

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp, ndiye aliye fanikisha Mo Salah kusaini mkataba mpya. Klopp muda mwingi alikuwa akiongea na Salah na kumweleza mipango ya baadae aliyo nayo kuijenga Liverpool, ‘kupitia yeye’. 

Salah ndiye mchezaji atakaye kuwa anaongoza kwa kulipwa pesa nyingi ndani ya kikosi cha Liverpool ’baada ya kukubali kulipwa mshahara wa £350k kwa wiki.

Mo salah sasa anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji ghari anaye lipwa fedha nyingi katika klabu ya Liverpool tangu kuanzishwa klabu hiyo.


Post a Comment

0 Comments