Ticker

6/recent/ticker-posts

Messi Atishia Kuondoka PSG, kisa Cristiano Ronaldo

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


RIPOTI zinaeleza kuwa, staa wa Paris Saint-Germain, Lionel Messi, ametishia kuondoka kikosini hapo endapo klabu hiyo itamsajili Cristiano Ronaldo.

Kwa sasa Ronaldo anatajwa kuondoka Manchester United, huku PSG ikiwa ni kati ya timu ambazo zinatajwa kumuwania sambamba na Chelsea na Bayern Munich.

Imeelezwa kuwa, hakuna uhakika kama PSG itatishika na suala hilo la Messi kwani timu hiyo inataka kujipanga kuona inafanya kweli katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini imeelezwa kuwa, uwepo wa Kylian Mbappe kwenye projekti mpya kunaweza kumvuta Ronaldo ndani ya kikosi hicho, Messi na Ronaldo wamekuwa washindani wakubwa kwenye soka ambapo wanatajwa kuwa ni wachezaji wenye rekodi za kutisha.

Ronaldo anashika nafasi ya pili kwa wachezaji wenye Ballon D’or nyingi akiwa nazo tano, huku Messi akiongoza akibeba saba.

Post a Comment

0 Comments