Ticker

6/recent/ticker-posts

Manchester United wakamilisha Usajili wa Tyrell Malacia

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Man United Yakamilisha Usajili wa Malacia, Yahamishia Nguvu kwa De Jong


KLABU ya Manchester United imekamilisha Usajili wa mlinzi wa kushoto kutoka klabu ya Feyenoord ya nchini Uholanzi Tyrell Malacia kwa ada ya paundi milioni 12.9 ambayo inatarajiwa kupanda hadi kufikia paundi milioni 14.6 kwa kipindi cha miaka mine (4) huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja zaidi.

Malacia alikuwa akigombaniwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Totenham Hotspurs.

Malacia mwenye umri wa miaka 22 anatajwa kuwa pendekezo la kocha mkuu wa klabua hiyo Erik Ten Hag ambaye amemfutailia kwa karibu tangu akiwa nchini Uholanzi.

Malacia anachangia wakala HCM Sports Management pamoja na kiungo raia wa Uholanzi Frenkie De Jong wa Barcelona ambaye naye anatajwa kukaribia kujiunga Old Trafford

Post a Comment

0 Comments