Ticker

6/recent/ticker-posts

Manara Nipo Tayari Kufungwa Miaka Kumi

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Yanga Haji Manara Niko Tayari Kufungwa Miaka Kumi

Msemaji wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa hahitaji kupata huruma kutoka kwenye mamlaka kutokana na kuweza kupewa adhabu ya kufungiwa miaka miwili pamoja na adhabu ya faini ya milioni 20 bali anahitaji haki.

Julai 21,Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) iliweka wazi kuwa imemfungia Manara miaka miwili pamoja na adhabu ya milioni 20 kutokana na kukutwa na hatia ya kumdhalilisha na kumdhihaki Rais wa TFF, Wallace Karia.

Manara amebainisha kuwa anatambua na kuheshimu mamlaka ambazo zipo lakini ambacho anahitaji ni haki na hahitaji kuonewa huruma kwa kile ambacho kinatajwa kwamba yeye amekifanya.

“Nimepewa hukumu ambayo ninadhani ni kubwa kuwahi kutokea kwa hivi karibuni kwenye ulimwengu wa mpira hasa adhabu ya faini ina maana kwamba nimefanya kosa kubwa kweli na la kutisha.

“Lakini yote haya hata mchango mdogo ambao nimeufanya kwenye mpira nadhani upo ikiwa ni pamoja na kuwa kwenye Kamati ya Hamasa ya Timu ya Taifa lakini nafanya yote haya sio kuomba huruma hapana ninataka haki iweze kutendeka.

“Ninajua kwamba sijafanya jambo baya na kama ikitokea basi acha iundwe kamati huru katika hili na ikitokea nikakutwa nimefanya makosa basi nipo tayari kufungwa jela miaka 10,” amesema.

Post a Comment

0 Comments