Ticker

6/recent/ticker-posts

Man Utd waongeza dau mbaka €50m kwa beki Lisandro Martinez wa Ajax

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Man Utd waongeza dau mbaka €50m kwa beki Lisandro Martinez wa AjaxManchester United wametuma ofa mpya ya €50m kwenda kwa Ajax kwajili ya Lisandro Martinez, United wana matumaini ya kushinda mbio za kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina dhidi ya mahasimu wao wa ligi kuu (Premier League) Arsenal.

Martinez amekuwa chaguo namba moja kwa kocha Erik Ten Hag baada ya United kumkosa beki Jurrien Timber, waliokuwa wanamuhitaji pia kutoka Ajax , Martinez amesha waambia Ajax nia yake ya kutaka kuondoka klabuni hapo kabla ya msimu mpya kuanza.

Sasa maamuzi juu ya kukubali au kukataa ofa hiyo yanabaki mikononi mwa bodi ya usajili ya Ajax. United wanauwakika wa kukamilisha usajili wa beki huyo muda si mrefu baada ya kutimiza vigezo kuhusu ada ya uhamisho kwajili ya mchezaji huyo. taarifa za kina ni kwamba mipango kwajili ya kumfanyia vipimo vya Afya beki huyo Ipo tayari.Post a Comment

0 Comments