Ticker

6/recent/ticker-posts

Man Utd wamefikia makubaliano ya kumsajili Lisandro Martinez kwa €55m

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

Man Utd wamefikia makubaliano ya kumsajili Lisandro Martinez kwa €55m

Manchester United Wamefikia Makubaliano na Ajax kwajili ya kumsajili Lisandro Martinez.

Hapo awali United walituma ofa mbili kwa Muargentina huyo, ambaye ana uwezo wa kucheza beki wa kati, beki wa pembeni na nafasi ya kiungo wa kati, na wamekuwa wakitaka kukamilisha dili hilo haraka iwezekanavyo huku Arsenal nao wakiwa bado wanamuhitaji.

Ajax wamekuwa na msimamo kwenye mazungumzo na United, na wamejaribu kuongeza dau mara kadhaa, lakini meneja Erik ten Hag amekuwa na hamu ya kumuona mchezaji huyo akijiunga nae tena Old Trafford hivyo imesababisha mazungumzo kuendelea.

Makubaliano yamefikiwa kati ya United na Ajax, huku washindi hao mara 13 wa Ligi Kuu ya Uingereza wakikubali kulipa ada ya €55m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 - €50m zitalipwa kama malipo ya uhamisho na €5m kama malipo ya nyongeza. 

Ajax walikuwa tayari kuongeza dau hilo la usajili mbaka kufikia €60m, lakini Martinez akawaambia anataka kujua mstakabali wake ndani ya saa 48 zilizopita - hivyo kusababisha mpango huo wa kuongeza dau hilo kuto fanikiwa.

Pia kumekuwa na mazungumzo yanayoendelea kati ya Chelsea na Ajax, Chelsea wakimuhitaji fowadi wa Ajax Antony ambae ni  Mbrazil, lakini vilabu hivyo viwili vimeshindwa kufika muafaka kwa sababu Ajax wanataka €80m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, hivyo bado muafaka haujafikiwa juu ya dili hilo.

United bado wanamuhitaji kiungo wa kati wa Barcelona Frenkie de Jong, wanajitahidi kufanya kila linalo wezekana kumpata, na sasa mtendaji mkuu Richard Arnold na mkurugenzi wa kandanda John Murtough wamesafiri kwenda Uhispania mapema wiki hii kujaribu kufanikisha swala hilo.

Kuna matumaini pia Christian Eriksen akasaini mkataba wa miaka mitatu hivi karibuni - kwa kuwa amechagua kujiunga na United badala ya kubaki Brentford.

Post a Comment

0 Comments