Beki huyo wa kimataifa wa Argentina amecheza mechi 177 katika klabu yake ya Ajax.
Ameshinda mataji mengi, ikiwa ni pamoja na taji la Copa America 2021 akiwa na timu ya taifa na mataji mawili ya Eredivisie akiwa na Ajax.
Lisandro Martinez akihojiwa kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na United amsema: "Ni heshima kubwa kwangu kujiunga na klabu hii. Nimejituma sana hadi kufika hapa,na kwa kuwa sasa niko hapa, nitajituma zaidi.
"Nimekuwa na bahati ya kuwa katika sehemu ya timu zilizofanikiwa katika maisha yangu na hilo ndilo ninalotaka kuendelea nalo hapa Manchester United. Kutakuwa na kazi ya ziada kufika hatua hiyo, lakini ninaamini kabisa kwamba, chini ya meneja huyu na makocha, kwa pamoja na wachezaji wenzangu, tunaweza kufanikiwa.
“Napenda kuwashukuru Ajax na mashabiki wao kwa sapoti waliyonipa. Nilikuwa na wakati mzuri sana nilipo kuwa nao lakini nahisi sasa ni wakati wa kujaribu kile nilicho kifanya nikiwa huko kukifanya katika mazingira mapya. Sasa niko kwenye klabu bora kufanya hivyo.”
Mkurugenzi wa soka wa Manchester United bwana john Murtough aliongeza kwa, kusema: “Lisandro ni mchezaji bora ambaye ataleta ubora na uzoefu zaidi kwenye kikosi cha Erik [Ten Hag].
"Tunafuraha kwamba amechagua kujiunga Manchester United na tunatarajia kumuona akiendelea mbele zaidi na kuisaidia timu kufikia mafanikio tunayolenga."
0 Comments