Ticker

6/recent/ticker-posts

Leeds wakubali ofa ya Barcelona

KLABU Ya Barcelona Imetuma  Ofa ya €58M na nyongeza ya €10M kwa Leeds United kwa ajili ya kumsajili Raphinha mwenye umri wa miaka 25. Leeds wamekubali ofa hiyo, na masuala binafsi kati ya Mbrazil huyo na Barcelona yalisha fanyika miezi minne iliyopita. 

Hapo awali Raphinha aliwapa Barcelona masaa 48 wawe wamekamilisha usajili huo la sivyo angeachana nao.


Dili hilo lipo katika hatua za mwisho baada ya Barcelona kutuma ofa kubwa kuliko ile iliyo tumwa na Chelsea na kutolewa nnje wiki mbili zilizopita… Raphinha kila mara alimwambia wakala wake Deco kwamba anataka kuhama Barca, na si kwingineko.


Post a Comment

0 Comments