Ticker

6/recent/ticker-posts

Kipre Junior na Tape Edinho watua Azam

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

 Azam yaanza kushusha vifaa


SIKU chache tu baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kumalizika, klabu ya Azam Imeanza kujiandaa na michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na maandalizi ya msimu ujao kwa kusajili wachezaji wawili kutoka nchini Ivory Coast. 

Klabu hiyo juzi jioni iliwatambulisha wachezaji Kipre Junior ambaye ni mshambuliaji na kiungo mshambuliaji Tape Edinho, kila mmoja akisajiliwa kwa mkataba wa miaka mitatu.

Taarifa zinasema kuwa mmiliki wa klabu hiyo, Yusuph Bakhresa ameamua kuingia mwenyewe mstari wa mbele kwenye usajili, kuhakikisha timu hiyo inarejesha makali na heshima yake kama miaka ya nyuma.

"Mashabiki zangu na mashabiki wa Azam FC, nimeamua, sasa mtafurahi sana." Ni kauli ya mmiliki huyo aliyoitoa wakati wa utambulisho wa wachezaji wao.

Klabu hiyo imewatambulisha rasmi wachezaji hao na kuandika kwenye mtandao wao rasmi wa instagram.

"Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Kipre Junior.”

Nyota huyo aliyekuwemo kwenye kikosi bora cha msimu huu wa Ligi Kuu ya Ivory Coast, amewahi kusajiliwa na miamba ya Ufaransa, Strarsbourg msimu wa 2017/2018. Aliwahi kuwatumikia vigogo wa Ivory Coast, Asec Mimosas, 2018-2020.

“Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeinasa saini ya kiungo mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Tape Edinho, kwa mkataba wa miaka mitatu.

“Edinho tumemnunua kutoka timu ya ES Bafing ya kwao, ambapo mkataba huo utamfanya kuhudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025.”

Nyota huyo mwenye uwezo mkubwa, amesaini mkataba huo mbele ya mmiliki wa timu hii, Yusuf Bakhresa  na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'.

Mkali huyo amechaguliwa kwenye kikosi bora cha Ligi Kuu ya Ivory Coast msimu huu kutokana na ubora wake wa kuhenyesha wachezaji wa timu pinzani.

Msimu uliomalizika, amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matano na kuchangia pasi tisa zilizozaa mabao." ilimaliza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments