Ticker

6/recent/ticker-posts

Kibwana atangaza vita Yanga........ "nitaonyesha nilichonacho kuisaidia timu kufanya vizuri"

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa


BEKI wa Yanga, Kibwana Shomari ametangaza vita baada ya kusema hana wasiwasi na ujio wa beki Joyce Lomalisa kwenye kikosi hicho.

Kibwana mwenye uwezo wa kucheza beki wa kulia na kushoto, msimu uliopita alicheza zaidi kushoto na kuwaweka benchi Yassin Mustapha na David Bryson ambao baadaye walikuwa wanasumbuliwa na majeraha.

Ujio wa Lomalisa unatishia uwezekanao wa Kibwana kupata namba lakini ametamka kwamba kila mmoja atumie vizuri nafasi anayopewa.

“Ni kitu kizuri kuja kwake kwenye timu, mimi nikipata nafasi nitaonyesha nilichonacho ili kuisaidia timu kufanya vizuri,” alisema Kibwana na kuongeza;

“Kweli wameimarisha eneo hilo na lengo ni timu kupata mafanikio na hilo sio suala geni kwenye mpira kwani mtu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ni kawaida.”

Kuhusu kucheza nafasi mbili tofauti alisema; “Kama mchezaji unatakiwa unapopewa nafasi tofauti na uliyozoea basi unatakiwa kumsikiliza kocha nini anakuambia na ufuate maelekezo, naamini nilifuata maelekezo ndio maana nikawa nacheza.”

Kibwana baada ya kufanya vizuri akiwa Yanga, kocha mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen alianza kumjumuisha kwenye kikosi chake.

Post a Comment

0 Comments