Ticker

6/recent/ticker-posts

Juventus wathibitisha kumsajili Paul Pogba kwa uhamisho huru

Kwa maombi ya kazi, Bofya hapa

  •  Juventus wathibitisha kumsajili Paul Pogba kwa uhamisho huruJuventus wamethibitisha kumsajili tena Paul Pogba kutoka Manchester United kwa uhamisho huru.

Mfaransa huyo aliondoka Old Trafford mwishoni mwa mwezi Juni kufuatia miaka miwili ya misukosuko akiwa United, Pogba anarejea Turin kwa mara ya pili katika maisha yake ya soka.

Hapo awali timu kama PSG, Real Madrid na Manchester City walionyesha nia ya kumuhitaji Pogba. Lakini Juventus walitangaza kwamba wamefanikiwa kupata saini yake, siku chache baadae alipigwa picha akikamilisha vipimo vya afya katika Uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.

Hatimaye katika taarifa yao ya wazi, Juventus wamethibitisha kwamba: "Paul amerejea Turin. Aliondoka kama kijana na anarejea kama mtu mzima na bingwa, lakini kuna jambo moja ambalo halijabadilika - Bado anakazi ya kuandika historia na klabu kwa mara nyingine tena."

Pogba atavaa jezi namba 10 ambayo aliivaa  kipindi cha mwishoni akiwa Juventus.

Post a Comment

0 Comments